Kumekuwa na utata mwingi kuhusu uungu wa yesu na watu wengi wanaopinga ni kwa sababu hawajishughulishi na kusoma neno LA mungu.kuna mafungu mengi ambayo yanadhibitisha kuwa yesu ni mungu.na somo hili limekuwa na utata wa Siku nyingi.
Leo fuatana nami kujifunza kuhusu yesu ni mungu sehemu ya kwanza. Yohana 10:30.yesu mwenyewe anakiri kwa kinywa chake.
Mimi na baba tu umoja. Pia yohana 14:6,7,8,na 9.
Katika mafungu haya yesu alijidhihirisha wazi wazi tena kwa msisitizo ya kuwa yeye ni Mungu. Mwanafunzi mmoja jina lake Filipo kauliza kwa Yesu tuonyeshe baba yatosha.Yesu akajibu nimekaa nanyi siku zoote hizo wewe usinijue pilipo ukiniona Mimi tayari umemuona Baba wewe wasemaje nikuonyeshe baba.?yohana 14:9 . pia nabii isaya alitabili wazi ya kuwa maana kwa ajiri yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto mwanaume.naye ataitwa MUNGU MWENYE NGUVU isaya9:6. Isaya 7:14 mtoto alitabiriwa Emanuel akizaliwa na bikira. Pia katika ufunuo wa yohana 1:8 yesu anasema Mimi ni Alfa na omega mwanzo na mwisho aliyeko na atakaye kuja MWENYEZI. MPENDWA MSOMAJI NENO
LA Mungu limetuonya mahala pengi kinachotakiwa ni kuchukua hatua ya kumwamini yesu kiristo na kumpokea na kujitenga na roho zidanganyazo ya kuwa yesu sio Mungu 1yohana4:1 yapasa kuzijaribu hizo roho kama zimetokana na mungu au LA. Maana mpinga kiristo ni yeye asemaye ya kuwa yesu sio mungu. Utukufu una yeye milele na milele amina! Kama una swali ushauri au maoni toa comment yako hapa chini pia usisahau kututembelea ktk blog yetu. Wabeloyablog.blogspots.com
Give Your Comment

Post a Comment